BREAKING NYUZZZZZZ.......: MLIPUKO MKUBWA WATOKEA JIJINI ARUSHA




Mungu uwe upande wetu

Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mara tu baada ya tukio hilo

eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....

Eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu  kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....


Na Ahmed mahmoud wa Globu ya Jamii, Arusha
MTU mmoja ambae hajafahamika jina lake ameuwawa , mtoto mmojayu  mahututi na wengine zaidi ya 49  wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka kitu kinachosadikiwa ni bomu majira ya saa  4 asubuhi leo  wakati wa sherehe za ufunguzi  wa kanisa jipya la Mt joseph,la Roman Katoliki, lililopo Olasiti jijini Arusha.



Ufunguzi wa kaisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisco  Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat  lebulu,  na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.

Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za  maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina  Fredirik, Joram  kisera, Novelt  John, Rose  pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt  John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .

Wengine ni Rioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim 


Mkuu wa mkoa wa  Arusha, Magesa Mulongo ,  ameagiza vyombo vya ulinzi na  usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.



Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka

Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..


Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.


 Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.

Previous Post Next Post