Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s akisindikiza kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (katikati). Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari aliyeambatana na Bi. Irina Bokova’s nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili iliyomalizika jana.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj akisalimiana na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji kwenye hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro wakati Balozi Begum Taj akisubiri kumsindikiza Airport Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO aliyeondoka nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea jijini Paris. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen.(Picha zote na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo akisalimiana na Mh. Mohammed Dewji.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s akielekea kwenye gari la maalum tayari kwa safari ya Airport.
Bi. Irina Bokova’s akiwasili VIP Terminal na kulakiwa na Bi. Rahma wa Ofisi za Unesco Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.Irina Bokova’s akizungumza jambo na Mh. Mohammed Dewji walipokutana Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mw. Julius Nyerere VIP Terminal. Kushoto ni Msaidizi wa Mh. Dewji Bw. Cosmas Mtesigwa na Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mh. Begum Taj.
Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s aliyeondoka nchini usiku wa kuamkia leo baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.
Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Kitengo cha Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka akipkea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo kabla ya kuondoka nchini usiku wa kuamkia leo.
Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo alifanya hivyo pia kwa Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari hii ikionyesha jinsi gani watanzania walivyokuwa wakarimu kwa wageni.
Safari ya kuelekea kupanda ndege iliwadia…..Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akiteta jambo na Bi. Irina Bokova’s wakati akimsindikiza kupanda ndege ya shirika la KLM usiku wa kuamkia leo.
Mama Rahma wa Ofisi za Unesco Tanzania akigana na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Kitengo cha Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka pamoja na Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari (kulia).
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen wakiwa ndani gari maalum linalowapeleka sehemu ilipopaki ndege ya shirika la KLM.