PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI LA MT. JOSEPH MFANYAKAZI, PAROKIA YA OLASISI YA JIJINI ARUSHA





Hili ndilo kanisa la Mt Joseph lililoko kwenye parokia ya Olasisi iliyoko katika jiji la Arusha

Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea

Ulinzi umeimarishwa


Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.


Hali ya eneo mlipuko ulipotokea


Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio


Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh Gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.




Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi. 



Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi. 





Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo. 



Hivi ni baadhi ya viatu vya watu waliokuwa wanakimbia mlipuko wa bomu lililolipuka nje ya kanisa ilo 







Gari la usalama likiingia eneo latukio 









Hawa watoto wakiwa wamepumzika baada ya kukimbia kutokana na bomu lililolipuka nje ya kanisa
























Previous Post Next Post