RODGERS: SUAREZ ANABADILIKA, HASTAHILI ADHABU YA KUFUNGIWA MECHI 10!!


Kocha wa wekundu wa Anfield, klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers ameeleza kuwa nyota wake Luis Suarez amejitahidi kubadili tabia yake na anahitaji msaada ili kurudi uwanjani na si kufungiwa mechi kumi na chama cha soka nchini England FA kwa kosa la kumng`ata mkono beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.

Liverpool walichanganyikiwa baada ya nyota wake kufungiwa mechi nyingi kiasi hicho baada ya FA kupata video ya tukio hilo ambalo halikuonwa na mwamuzi katika mchezo wa timu hizo jumapili ya wiki iliyopita.

Suarez bado ana muda wa kukata rufaa mpaka kesho, lakini Rogers alisema nyota wake amehukumiwa adhabu kubwa sana na FA iangalie upya kwani atarekebisha makosa yake.




Rodgers alisema” Tumeshistushwa na maamuzi makubwa kiasi hicho, hakika tumeumizwa sana, licha ya kuwa mchezaji wetu, Luis alionekana kujutia kosa lake na alikubali kuwa amefanya makosa”.


Anatabasamu: Luis Suarez akifanya mazoezi siku aliyopewa adhabu ya kufungiwa mechi 10 na FA.

 

 
Leo hii: Suarez ameonekana mwenye moyo wa kijasili wakati anafanya mazoezi mchana wa leo.



 
Hapa Ivanovic alikuwa anamweleza mwamuzi wa mechi yenyewe Kevin Friend kwamba Luis amening`ata Ivanovic 

Previous Post Next Post