MIKE TYSON HAONI HATARI KITENDO ALICHOFANYA LUIS SUAREZ




Aliyekuwa bondia wa kimataifa, Mike Tyson ameendelea kuwashangaza wengi hasa baada ya kuendelea kuonyesha hisia zake za kumsapoti mchezaji wa Liverpool, Luis Suarez kwa kitendo chake cha kumn’gata mchezaji mwenzake uwanjani juzi.

Baada ya kuvuta attention ya watu kwa kumfuata mchezaji huyu katika mtandao wa Twitter, Tyson wakati akijibu swali juu ya hatua yake hii amesema kuwa mambo kama haya hutokea na ana hakika kuwa Suarez amekwisha elewana na Ivanovic kama yeye aliweka mambo sawa na Evander baada ya kumng’ata sikio mwaka 1997.

Tyson ameweka sawa kuwa, amemfuata mchezaji huku katika mtandao si kwa ajili ya kuunga mkono vitendo vya ung’ataji, ila amefanya hivyo kwa lengo la kumfahamu zaidi yeye pamoja na visa vyake vya ung’ataji.

Previous Post Next Post