HIVI NDIVYO WATAVYOMUENZI NELSON MANDELA!





Katika kutambua mchango na nafasi ya mwanaharakati mkongwe na mpigania haki na uhuru Nelson Mandela, Huko Marekani, Times Square New York kutakuwa kukionyeshwa kwa picha pamoja na nukuu za shujaa huyu wa Afrika katika mabango ya kielektroniki.
Hii ni hatua moja kubwa ya kuenzi na kusherekea kuelekea kutimiza miaka 95 kwa Mandela mwezi July mwaka huu, na nukuu ambazo zitakuwa zikionyeshwa ni kazi ambayo imefanywa na Ndaba, Mjukuu wa mzee huyu ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30.
Mpango huu umefadhiliwa na Tribeca Film Institute ambayo ni taasisi ya sanaa iliyoanzishwa kwa ushirikiano na mwigizaji maarufu mwenye rekodi ya kushinda tuzo za Oscar, Robert De Niro
Previous Post Next Post