Mwaka 2013 ni mzuri kwa rapper Nay wa Mitego. Licha ya kuwa na hit single hewani, Muziki Gani aliyomshirikisha Diamond, rapper huyo amenunua ndinga mpya aina ya Mark X yenye thamani ya shilingi milioni 35. Kama hiyo haitoshi, hitmaker wa Nasema Nao, amejihami pia kwa kununua bastola.
![]() |
NEY WA MITEGO |

Nay akiwa na bastola yake
Nay ameshare picha hizo kwenye Instagram na Facebook ambapo miongini mwa picha za gari lake ameandika, ‘My new car. Mark X, Zic z wat I nid.” Mwaka huu Nay ametumiwa kwenye show nyingi za Airtel na Vodacom ambazo huenda zimemwingizia mkwanja wa kutosha.




