FERGUSON ATAJWA KOCHA TAJIRI ZAIDI UINGEREZA!!

Baada ya kutwaa ubingwa wa 20 na klabu ya Manchester United, Bosi wa mashetani hao wekundu, Sir Alexandar Chapman Ferguson “Kibabu Fergie” ametajawa tena katika tuzo nyingine ya kocha tajiri zaidi katika soka la England kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na gazeti la Sunday Times.
Ferguson ameshinda taji ya kuwa kocha tajiri zaidi akifuatiwa katika nafasi ya pili na aliyekuwa kiungo wake Old Trafod Roy Keane huku mzee Arsene Wenger akiwa nafasi ya tatu.
Kibabu ametajwa kuwa kocha tajiri zaidi England akiwa na kitita cha pauni milioni 34 katika akaunti yake.
Tuzo nyingine: Sir Alex Ferguson kocha tajiri zaidi kwa mujibu wa orodha ya gazeti la Sunday Times




Roy Keane alitengeneza pesa nyingi akiwa mchezaji na sasa anapata pesa nyingi tena akiwa mtangazaji wa ITV




Miaka kumi akiwa juu: Arsene Wenger ndiye kocha pekee anayelipwa dau kubwa zaidi nchini 
Naye kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson ambaye ana mkataba wa pauni milioni 3 kwa mwaka na chama cha soka England ameingia kumi bora akiwa na kitita cha pauni milioni 12, lakini anazidiwa na kocha aliyemrithi mikoba yake Sven Goran Eriksson aliyejikusanyia pauni milioni 16.
Kocha Manchester City  Roberto Mancini na wa Ireland Giovanni Trapattoni  wameingia pia katika orodha hiyo.
Pia kocha wa muda wa Chelsea Rafa Benitez yupo kwenye orodha hiyo akiwa na kitita cha Pauni milioni 12 licha ya mkataba wake kuwa mwishoni. 
MAKOCHA TAJIRI ZAIDI WA SOKA(Pamoja na makocha wa zamani wa timu za Uingereza)
RankingNameTeam2013 wealth2012 wealth
1Sir Alex FergusonManchester United£34m£32m
2=Roy KeaneEx Ipswich Town and Sunderland£29m£29m
2=Arsene WengerArsenal£29m£26m
4=Roberto ManciniManchester City£21m£18m
4=Giovanni TrapattoniIreland£21m£20m
6Sven-Goran ErikssonEx England and Leicester City£16m£16m
7=Steve BruceHull£14m£14m
7=Mark HughesEx-QPR£14m£11m
9Harry RedknappQPR£13m£12m
10=Rafa BenitezChelsea£12mNew
10=Roy HodgsonEngland£12m£11m
10=Martin O’NeillSunderland£12m£10m
Wakati huo huo Lewis Hamilton ametajwa kuwa dereva mwenye kitita kikubwa kuliko wote wa michezo ya Fumula One ambapo ana kitita cha Pauni milioni 60.
Nafasi ya pili imeshikwa na Jenson Button ambaye ana kitita cha  pauni milioni 5

Madereva tajiri zaidi wa  F1 wazaliwa wa Uingerza
RankingNameF1 Team2013 wealth2012 wealth
1Johnny DumfriesLotus£110m£110m
2Eddie IrvineFerrari£83m£80m
3Lewis HamiltonMercedes£60m£55m
4Jenson ButtonMcLaren£58m£53m
5Jody ScheckterFerrari£57m£60m
6David CoulthardMcLaren£53m£50m
7Nigel MansellWilliams£50m£50m
8Sir Jackie StewartTyrrell£42m£42m
9=Damon HillWilliams£19m£19m
9=Jonathan PalmerTyrrell£19m£22m
Previous Post Next Post