
Nyota huyo wa Amerika Kusini, alifunga bao hilo dakika ya 47 na sasa City itamenyana na Wigan katika fainali mwezi ujao. Lakini mshambuliaji huyo alinusurika kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu David Luiz.
Samir Nasri alitangulia kuifungia City dakika ya 34, lakini Chelsea ikasawazisha kupitia kwa Demba Ba dakika ya 67.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Pantilimon, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Y Toure, Barry, Milner, Tevez/Garcia dk71, Nasri/Lescott dk86 na Aguero.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Bertrand, Ramires, Mikel/Torres dk65, Hazard, Mata, Oscar na Ba.