Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi nchini (TSIA), Athuman Maige (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Isaya Maiseli. Viongozi hao walikutana na waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya chama hicho na wizara.
Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi nchini (TSIA), Athuman Maige (katikati) akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya chama chake na wizara hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Isaya Maiseli.
Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi nchini (TSIA), Athuman Maige (kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya chama chake na wizara hiyo.