KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA KAMPENI MPYA YA “TUKO PAMOJA KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO”


se1
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte wakati kampuni hiyo ilipotangaza rasmi kampeni mpa ya bia ya Serengeti Lager inayokwenda kwa jina la “Tuko Pamoja Katika Shangwe za Mafanikio”, katika picha kulia ni Mosses Keba Meneja Masoko wa Kampuni ya Serengeti na Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo
se3Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager  akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kampeni mpya ya bia hiyo inayoitwa “Tuko Pamoja katika Shangwe za Mafanikio”  kampeni inayoanza leo katika baa mbalimbali jijini Dar es saalaam Allan amezungumzia kampeni hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es saalaam , kulia ni Mosses Keba Meneja Masoko wa  bia ya Serengeti se2Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte wakati kampuni hiyo ilipotangaza rasmi kampeni mpa ya bia ya Serengeti Lager inayokwenda kwa jina la “Tuko Pamoja Katika Shangwe za Mafanikio” kutoka kulia ni Mosses Keba Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager na Kushoto ni Imani Lwinga Meneja Mawasiliano wa Serengeti
……………………………………………………………………..
Leo katika hafla iliyohudhuriwana waandishi wa habari, wageni na wadau mbalimbali Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni mpya na ya kipekee inayoenda kwa kauli mbiu ya TUPO PAMOJA.  Katika hafla hiyo iliyofana asubuhi ya leo pia ilihudhuriwa na wadau wa bia hii katika ishara ya kushereheka mafanikio na shangwe za bia hii.
 Akiongea na waandishi wa habari asubuhi la leo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia Serengeti Bw. Ephraim Maguru alisema kwamba, “ kwa miaka kumi saa, tumeona na kushuhudia ukuaji na mafanikio makubwa”.  Bia hii inajulikana kwa kampeni ya ‘raha kamili kwa wengi wanaifahanu kama Chui.  Pia kwa udhamini wa Taifa stars ambao uliinua hadhi ya soka la Tanzania kwa kiwango kikubwa.  Kuna ufadhili wa Fiesta, ambao wote mnajua mchango Fiesta inatoa katika ukuaji wa tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini.  Aliendelea Bw. Mafuru
 Bia ya Serengeti ni bia ya kipekee ambayo ndio bia ya kwanza Tanzania yenye kimea halisi kwa asilimia mia.    Mwaka jana bia hii pia ilizindua muonekano mpya  wa nembo yake huku ikibaki na ladha ile ile.  Baada ya utafiti, Kampuni ya bia ya Serengeti na wadau wake, wamebaini kwamba watanzania wanahitaji  shangwe za mafanikio yao katika sekta mbalimbali zikiwemo za uchumi, kijamii, kimichezo na kadhalika.
 “Tunawakaribisha wote katika hafla mbali mbali ambazo tutaandaa ili kueneza kampeni hii ya Tupo Pamoja kama mlivyoona katika matangazo niliyowaonyesha, tutaleta shangwe popote mlipo., Alieleza meneja wa kinywaji hicho Bw. Allan Chonjo,  baada ya kuonyesha matangazo mbali mbali yatakovyokuwa katika vyombo vya habari.
 Hafla hiyo ya uzinduzi pia ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Kampuni ya bia ya Serengeti wakiwemo wasambazaji wa bia.  Kampeni hii inawatambua na kuwathamini  watanzania wote  kwa mafanikio yao katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Previous Post Next Post