UTEUZI WA BODI YA KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA ARUSHA (AICC)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua kwa kipindi kingine Balozi Christopher Liundi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa-Arusha (AICC).
Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.) amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kama ifuatavyo:-
1. Bw. Aggrey Mlimuka
2. Bw. Dash-Hood Mndeme
3. Dkt. Ali Mndali
4. Mhe. Balozi Abdi Mshangama (Mstaafu)
5. Mhe. Faith Mtambo (Mbunge wa Viti Maalum)
6. Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala (Mbunge wa Nzega)
7. Mhe. Mary Chatanda (Mbunge wa Viti Maalum)
8. Mhe. Ali Mzee Ali, (Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi – Zanzibar)
9. Bw. Wilson Masilingi (Mbunge Mstaafu) 
Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 06 Machi, 2013.   
IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE  NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM
8 MACHI, 2013.
Previous Post Next Post