WAZIRI NCHIMBI AFUNGUA MAFUNZO


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akipokelewa na Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia kwa wakuu wa magereza wa mikoa yote Tanzania Bara, maafisa waandamizi wa makao makuu, watumishi raia na askari kutoka magereza mbalimbali nchini. Mfunzo hayo ya siku nne yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ili afungue mafunzo ya jinsia kwa maafisa magereza nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na maafisa mbalimbali wa jeshi la magereza kabla ya kufungua mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi hilo, Deonis Chamulesile.
Maafisa Magereza wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya jinsia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia) akimshukuru Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta baada ya kumkabidhi taarifa ya hali ya Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia katika  Taasisi zinazotekeleza Programu ya Maboresho ya Sekta hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa katikati waliokaa) akiwa na Wakuu wa Magereza ya Mikoa yote ya Tanzania Bara  katika picha ya pamoja.

Previous Post Next Post