Seneta wa zamani wa Massachusets na mwenyekiti wa zamani wa kamati ya mambo ya nje ya baraza la seneti akiapishwa rasmi kuwa waziri wa mambo ya nje huku mke wake, Teresa Heinz Kerry akiangalia.
Waziri mpya wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amepiga simu zake za kwanza kwa viongozi wa nje akiwa kama mwanadiplomasia wa juu wa Marekani.
Wizara ya mambo ya nje inasema Kerry amempigia simu waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas jumapili. Aliwaambia wote kuwa anaahidi kufuatilia binafsi suala la amani Mashariki ya Kati . Pia alisema maamuzi ya kuachia faida ya kodi ni hatua nzuri.
Wizara ya mambo ya nje inasema Kerry aliwapigia mawaziri wa mambo ya nje wa Canada, Mexico na Uturuki siku ya Jumamosi. Pia amekutana na kuzungumza na kila waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani aliye hai akitaka ushauri wao.
John Kerry aliapishwa Ijumaa iliyopita kama waziri wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Hillary Clinton aliyeomba kustaafu baada ya kutumikia serikali ya Marekani kwa muda mrefu.