VIJANA TANZANIA AWATAKIWA KUTUMIA VIZURI UJASILIAMALI


Aliongeza kuwa ili ujasiriamali ufanikiwe, vijana wanatakiwa kwanza kuwa na mwamko wa kujitegemea na elimu ya kujitgemea wanapoipata inawasaidia kupambana na changamoto. 
VIJANA wametakiwa kuitumia vyema elimu ya ujasiriamali wanayopata kuendesha biashara zao ili kuboresha vipato vyao na kujikwamua na umaskini.

Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Ilala, Profesa Elisante Gabriel alipotoa mada kwenye semina ya ujasiriamali.
Profesa Gabriel alisema vijana Watanzania wengi hawajitumi kuwa wajasiriamali, licha ya elimu wanayoipata.
Aliongeza kuwa ili ujasiriamali ufanikiwe, vijana wanatakiwa kwanza kuwa na mwamko wa kujitegemea na elimu ya kujitgemea wanapoipata inawasaidia kupambana na changamoto. Alisema miradi mingi inayoanzishwa Tanzania inakosa mipango ya maendeleo siyo mitaji, aliwataka vijana kuacha kulalamikia ukosefu wa mitaji kama kisingizio.

Profesa Gabriel alisema vijana wafikirie jinsi ya kuendeleza miradi mbalimbali wanayoanzisha kutokana na mitaji midogo wanayopata.
Pia, aliwataka vijana kuwa wabunifu na kutofanya shughuli za kuigana, kuangalia mahitaji ya masoko jambo ambalo litasaidia kufanikiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi aliwataka vijana kutokubali kushindwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kwamba, wanatakiwa kujituma zaidi kutimiza malengo yao.

“Kila mmoja wetu atambue kwamba huu ni wakati mzuri wa kupanga mikakati ya biashara, imepita zaidi ya miaka 20 na wakati wa kutekeleza ni sasa, nikimaanisha biashara zote zinazofanywa sasa zilipangwa tangu miaka 20 iliyopita kinachofanyika sasa ni utekelezaji tu,” alisema Mushi.

Pia, aliwataka vijana pia kujitambua na kutambua malengo yao mapema, ili kujipangia muda wa kuyatekeleza na kuyafikia hatimaye kufanikiwa.



Previous Post Next Post