BAADHI ya waganga wa kienyeji nchini sasa wamegeuza matatizo ya Watanzania kuwa mitaji yao ya kujipatia mamilioni ya fedha kwa madai kwamba wanawapatia tiba.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumamosi umebaini kuwa wengi wa waganga hao wanaojipatia fedha kwa njia ya kuwadaganya wananchi ni wale ambao hawajasajiliwa na Serikali. Moja ya uthibitisho wa kwamba huduma hiyo haramu huwapatia fedha nyingi waganga hao ni kuenea kwa mabango mengi yanayotangaza kuwepo kwa waganga hao.
Katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam na miji migine mikubwa nchini huwezi kutembea mwendo mrefu bila kukutana na kibao kinamtangaza mganga wa kienyeji kutoka ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa waganga hao, wapo wanaojitangaza kutibu watu walio na matatizo ya nguvu za kiume, wanaotaka kupata utajiri wa haraka, kutibu mwanafunzi ambaye hana akili darasani, kuolewa au kuoa haraka, kumvuta mpenzi aliye mbali, kunenepesha makalio na kurefusha maumbile ya sehemu za siri kwa wanaume na mengineyo.
Wingi wa matangazo hayo unaashiria pia kuwapo kwa watu wengi wenye matatizo na wanaotumia huduma hizo, ambao huwasiliana na waganga hao kwa njia ya simu zilizoandikwa kwenye matangazo yao ya kuvutia wateja. Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi Jumamosi umebaini kuwa waganga hao wengi ni feki, ambao hawana tiba hiyo, badala yake wanajipatia mamilioni kutoka kwa wananchi hao wakiwaachia madhara, pengine kusababisha vifo.
Baadhi ya waganga hao, ambao wanaweka mabango yao jijini Dar es Salaam kutangaza tiba yao ni lile linalosomeka Dk .. wa Nigeria anatibu matatizo akili darasani, mafanikio siku tatu, kukuza uume, kung’arisha nyota, makalio na magonjwa mengine.
Tangazo jingine la mganga wa kienyeji linalosomeka : “Dk … anatibu, ugumba, nguvu za kiume, mvuto wa mapenzi, kumwita mpenzi aliye mbali na utajiri wa haraka.”
Yapo matangazo mengine ambayo yanaonyesha kuwa wanatoa huduma mbalimbali ikiwamo kurejesha fedha ambazo mtu alidhulumiwa, kulipiza kisasi kwa mtu aliyekukosea, kupata nguvu za ajabu katika kufanya mapenzi, kutibu Ukimwi, saratani, mabusha, magonjwa wa zinaa na kupata utajiri kwa siku mbili.
Katika uchunguzi wake Mwananchi Jumamosi liliwasiliana na waganga wawili mmoja akijitaja kuwa ametoka Nigeria akiwa na ofisi zake Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam na kuzungumza naye kwa simu ya mkononi kujua namna anavyotoa tiba yake na mazungumzo yalikuwa hivi
Mwananchi Jumamosi: Halo Dk Abuja, nimechukua namba yako katika tangazo la biashara zako, mimi nina shida!
Dk Abuja: Shida gani sema?
Dk Abuja: Shida gani sema?
Mwananchi Jumamosi: Nina mtoto wa dada yangu anasoma kidato cha pili, lakini ana matatizo ya kutoelewa darasani, gharama yake itakuwaje?
Dk Abuja: Inawezekana kabisa, gharama ni Sh 50,000, lakini naomba unitumie kwanza jina la mtoto huyo na unirushie Sh21,000 kwa njia ya simu sasa hivi, ili ni mwangalie kwanza huku.
Mwananchi Jumamosi: Sasa baada ya kumfanyia matibabu hayo anatakiwa kusubiri kwa muda gani?
Dk Abuja: Nakupa wiki moja tu, tena utashangaa mno, yaani atakuwa na uwezo wa kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne.
Mwananchi Jumamosi: Dk Abuja, vipi kuhusu mafanikio, nataka pesa bwana maisha magumu!
Dk Abuja: Kwa hilo, ukija hapa ofisini nitakueleza vizuri, inategemea gharama zake kwa sababu itanibidi kuangalia ukoo wako na kutimiza masharti ambayo siyo magumu.
Baada ya kumaliza mazungumzo na Dk Abuja, gazeti hili lilifanikiwa kumpata mganga mwingine analiyejiita bingwa wa kurekebisha nyota, maarufu anayepatika Tabata jijini Dar es Salaam, ambapo mazungumzo yalikuwa hivi;
Dk Abuja: Kwa hilo, ukija hapa ofisini nitakueleza vizuri, inategemea gharama zake kwa sababu itanibidi kuangalia ukoo wako na kutimiza masharti ambayo siyo magumu.
Baada ya kumaliza mazungumzo na Dk Abuja, gazeti hili lilifanikiwa kumpata mganga mwingine analiyejiita bingwa wa kurekebisha nyota, maarufu anayepatika Tabata jijini Dar es Salaam, ambapo mazungumzo yalikuwa hivi;
Mwananchi Jumamosi: Dk …nimepata namba yako ikanibidi nikutafute, nina shida mzee.
Dk Tabata: Kwanza wewe una miaka mingapi, haya tuendelee, una shida gani?
Mwananchi Jumamosi: Mimi ni mfanyabiashara, ninataka nyota yangu ing’ae. Je, gharama yake itakuwaje?
Dk Tabata: Gharama yake ni Sh100,000 na haitakiwi kupu ngua hata senti, kwa sababu wazee waliomba noti kumi katika tatizo hilo.
Mwananchi Jumapili: Nyota yangu itabadilika kwa kiwango gani mtaalamu?
Dk Tabata: Ni kwa kiwango kikubwa sana, unaweza kuzidi hata nyota ya Rais Jakaya Kikwete na Said Bakhresa, nakwambia utanitafuta mwenyewe tu baadaye.
Kuhusu usajili wao
Mbali na kukithiri kwa matibabu yanayotolewa na wataalamu hao, Kaimu Msajili Mkuu wa Tiba Asili na Mbadala nchini, Dk Naomi Mpemba anasema kuwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za usajili, waganga wote wanaojitangaza kutoa tiba hawaruhusiwi kufanya hivyo.
Akifafanua kuhusu utaratibu wa usajili waganga nchini, Dk Naomi anaeleza kuwa tangu mwaka 2011, Serikali imetoa agizo la kuwataka waganga wote nchini kujisajili ili watambuliwe rasmi taaluma na matitabu yao kwa jamii ili Serikali iweze kushirikiana nao.
Anasema kuwa tangu walipoanza usajili huo mwaka 2011 hadi Desemba mwaka uliopita, waganga 3,297 pekee ndiyo waliojisajili na wengine wengi wanafanya kazi kitapeli.
“Hata wenye majina makubwa bila kujali nani, tumewafuatilia na kujiridhisha kuwa wanadanganya jamii,” alisema Kaimu Msajili huyo.
Dk Naomi anaongeza kuwa mbali na kuonekana mitaani wakitoa huduma hizo, waganga wengi hawana usajili wa Serikali na kwamba mwitikio wao kufanya hivyo ni mdogo ikilinganishwa na idadi yao waliopo hasa wanaojitangaza.
“Mnavyoona matangazo mengi ya wanajiita wanatoka Sumbwanga hata Nigeria, waliosajiliwa hawafiki hata asilimia kumi, wanahofia huenda dawa zao zina shaka, hazifai kwa hivyo wanaamua kutumia nguvu ya kujitangaza ili kuuteka umma,” alisema Dk Naomi.
Alisema kuwa waganga hao wantumia mwanya wa matatizo ya jamii na kuwalaghai wananchi.
“Tumekuwa tukipiga kelele sana kwa Watanzania, lakini hawasikii,wanaibiwa na kudanganywa kama watoto,”alisema.
Dk Naomi aliongeza kuwa sheria na taratibu zinaeleza wazi kwamba waganga wote waliosajiliwa hawaruhusiwi kujitangaza.
”Hata wanaojiita kina waganga wa tiba asili wakubwa wanaoonekana kwenye televisheni, hawajasajiliwa. Tunawatambua kama ni feki kwa kudanganya watu wana tiba mbadala, wakati siyo kweli,”alisema Dk Naomi.
Agizo la Serikali
Kwa mujibu Dk Naomi ifikapo Machi mwaka huu, Bazaza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, litakuwa na vikao vya kamati ambapo watajadili kupitisha maazimio ya kudhibiti na kuboresha utoaji wa huduma hiyo nchini.
Alisema kwa sasa Serikali haiwezi kuandaa operesheni ya kuwasaka waganga hao, badala yake itakapofunga zoezi la usajili wao, ndiyo itaanza zoezi la ukaguzi huo kwa kila maeneo yote nchini. Alisema kuwa mbali na wasiokuwa na usajili, kwa waliosajiliwa taratibu na kununi za usajili zimekuwa zikitoa kibali cha muda wa miaka mitatu kama muda wa matazamio.
Daktari
Akizungumzia uwezo wa waganga hao kuongeza akili za darasani, Daktari wa Kitengo cha Kliniki ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Juma Mguta alisema kuwa kitaalamu akili za mwanadamu haziwezi kupandikizwa, badala yake kuna mfumo wa kurithi kutoka kwa wazazi pamoja na mazingira.
Akizungumzia uwezo wa waganga hao kuongeza akili za darasani, Daktari wa Kitengo cha Kliniki ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Juma Mguta alisema kuwa kitaalamu akili za mwanadamu haziwezi kupandikizwa, badala yake kuna mfumo wa kurithi kutoka kwa wazazi pamoja na mazingira.
“Mtoto anapozaliwa anaweza kurithi asilimia 40 ya akili kutoka kwa wazazi wake na asilimia 60 anaweza kuipata kutoka katika mazingira yanayozunguka, pamoja na taaluma yangu sijawahi kusikia mtu amepona kwa kutibiwa akili,”alisema Mguta.
Alisema kuwa kama kungekuwa na dawa inayotibu tatizo hilo basi Tanzania haipaswi kuwa na janga la watoto wanaofeli kwa kiwango kilichojidhihirisha katika matokeo ya mitihani mbalimbali nchini.
Dk Mguta aliongeza kuwa endapo kuna waganga wenye uwezo wa kuondoa tatizo hilo kitaalamu, wangejitokeza na kuisaidia jamii ya Kitanzania kwa lengo la kuo ndoa janga la ujinga.
Kiongozi wa dini
Akizungumzia hali hiyo Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kutoka Mbeya, Gwamaka Mwakilembe alisema kuwa jamii imechanganyikiwa kutokana na huduma zinazoendelea kuzagaa nchini.
“Watu wanaona upande wa Mungu kuna miujiza mingi inatolewa, lakini wanasikia pia kuna utapeli ndani yake. Hivyo hiyo kwa waganga hao wanakimbilia huko kwa kuamini watamaliza shida zao wakati matapeli ndiyo wanaongezeka,” alisema Mchungaji Gwamaka.
Alisema Serikali inaonekana kushindwa kudhibiti biashara hiyo kwa kuwa mabango yao kila mahali.
Wananchi
Mzee Joseph Bigelo (59), mkazi wa Tabata alisema kuwa asilimia kubwa ya waganga hao kwa sasa wamekuwa wadanganyifu. “Mimi iliwahi kunitokea, kipindi hicho nilimtafuta mganga kwa lengo kuniongezea nguvu za kiume, lakini baada ya kumpigia akaniomba kwanza nimtumie pesa kwa njia simu kisha anitumie dawa kwa njia usafiri wa basi,”alisema Bigelo.
Mzee Bigelo alisema hadi hatua ya mwisho wa mawasiliano yao, alifanikiwa kutambua mganga huyo alikuwa ni tapeli.
Naye mzee aliyejitambulisha kwa jina moja la Mgosi alisema kwamba baadhi ya waganga wamekuwa wadanganyifu na kusababisha wananchi kuondoa imani utoaji wa tiba mbadala na asilia.Alisema kwamba Serikali inapaswa kuingilia kati suala hilo kwani jamii itazidi kuangamia.
Majina ya waganga wa tiba asili yaliyotumika siyo halisi