Waziri wa Ujenzi Mhe. John Magufuli akimuaga Mke wa Waziri mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere VIP Terminal jijini Dar.
Waziri wa Ujenzi Mhe. John Magufuli akimuaga Waziri Mkuu wa Kenya Mhe. Raila Odinga kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwl. Julius Nyerere VIP Terminal jijini Dar.
Waziri wa Ujenzi Mhe. John Magufuli wakiagana na Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwl. Julius Nyerere VIP Terminal jijini Dar.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Odinga amerejea Nairobi baada ya kuwepo nchini Tanzania kwa mapumziko ya siku saba. Mheshimiwa Odinga alitumia muda wa mapumziko yake hapa nchini kutembelea maeneo mbali mbali ya kihistoria, mbuga za wanayama na visiwa vya Zanzibar ambako alisherehekea mwaka mpya.
Katika ziara hiyo binafsi, Mheshimiwa Raila Odinga aliambatana na Mkewe Mama Ida Odinga pamoja na wanafamilia wa karibu. Wakati akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Odinga alielezea kufurahishwa kwake na namna alivyoweza kupokewa na kupata muda mzuri wa mapumziko na kwamba sasa yuko imara kabisa kuendelea na majukumu yake ya kisiasa.
‘Nimepumzika vizuri na kusherehekea vyema mwaka mpya wa 2013 katika visiwa vya Zanzibar, ninawashukuru wote walioshirikiana na familia yangu na ninawatakia Heri ya Mwaka Mpya’ alimalizia Waziri Mkuu huyo wakati akiagana na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwepo uwanja wa ndege kumsindikiza