Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi klabu bingwa ya Tanzania bara timu ya Simba SC ya Dar leo imeanza vizuri mbio za kuutetea ubingwa wake wa Mapinduzi kwa kuichapa Jamhuri ya Zanzibar kwa mabao 4-2 katika mchezo ulioisha hivi punde huko visiwani.
Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na kinda Haruna Athumani Chanongo aliyepiga mawili, Felix Sunzu na Shomari Kapombe wakitupia kambani goli moja kila mmoja.
Jamhuri ndio walikuwa wa kwanza kuliona goli la Simba katika robo ya kwanza ya mchezo kwa goli lilofungwa na Mfanyeje Mussa, kabla ya Simba kusawazisha katika dakika ya 27, na baadae kidogo akaongeza bao la pili kwa shuti kali. Mfanyeje tena aliwaumiza tena Simba na timu zikaenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu.
Awamu ya pili ya mchezo Simba walirudi vizuri na kupata mabao mawili yaliyofungwa na Felix Sunzu na Shomari Kapombe na kuipa timu yao ushindi wa kwanza ndani ya mwaka 2013.