KLABU YA SHANGHAI KUWASILISHA PINGAMIZI LA UHAMISHO WA DROGBA FIFA



Klabu ya Shanghai Shenhua imesema kuwa Didier Drogba angali mchezaji wake na kuwa uhamisho wake hadi klabu ya Galatasaray inakiuka masharti ya mkataba wake.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea, amesaini mkataba wa miezi kumi na minane na klabu ya Galatasaray inayoshiriki katika ligi kuu ya Uturuki.
”Tumeshangazwa sana na tangazo hilo” Klabu hiyo ambayo ilimsaini Drogba kwa mkataba wa miaka miwili na nusu mwezi Julai mwaka uliopita, imesema.
”Drogba angali mchezi wa klabu ya Shanghai Shenhua kwa kuwa mkataba kati yao bado haujakamilika.
Klabu ya Galatasaray siku ya Jumanne ilitangaza kuwa Drogba atajiunga na klabu hiyo baada ya kukamilika na mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Afrika Kusini.
Lakini Shenhua imepinga uhamisha huo na kussema kuwa liko tayari kuwasilisha malalamishi yake ya shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.
Mchezaji hiyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini kuiongoza kikosi cha Ivory Coast katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.

Previous Post Next Post