TUNISIA WAAGA AFCON, TIMU YA TOGO KUONJA ROBO FAINALI



Mechi ya mwisho ya makundi kati ya Togo na Tunisia, moja ya mechi ngumu zaidi katika fainali za mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu imekamilika.
Timu hizo mbili zimetoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja na hivyo Togo imefuzu kutokana na idadi ndogo ya magoli waliyofungwa katika raundi hiyo ya kwanza, licha kuzoa alama nne sawa na Tunisia.
Tunisia ilihitaji ushindi katika mechi hiyo ili ifuzu kwa raundi ijayo huku togo nikihitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu kwa raundi ijayo.
Togo ilianza mechi hiyo kwa vishindo huku ikipata bao lake la kwanza kunako dakika ya 12 kupitia kwa mchezaji Serge Gakpe ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha wa timu hiyo Emmanuel Adebayor.
Kunako dakika ya 30 Tunisia ilizawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wake Walid Hichri kuangusha kwenye eneo la hatari na Dare Nibombe.

Previous Post Next Post