Hali ya wasi wasi imetanda katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Afrika ya kati, Bangui, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kufika mji huo, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umewahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo, nayo serikali ya Marekani imetoa wito kwa raia wao kuondoka nchini humo.
Serikali ya Ufaransa kwa upande wake imeagiza usalama kuimarisha katika ubalozi wake mjini Bangui, baada ya kushambuliwa na waandamanaji waliorusha mawe ya kuchoma bendera ya Ufaransa, Raia hao wanataka serikali ya Ufaransa kusiadia kuzima uasi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Ufaransa ina takriban wanajeshi mia mbili mjini Banguia na utawala wa nchi hiyo umetoa wito kwa Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kukabiliana na wanajeshi wa waasi ambao wameuteka maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo. Lakini rais wa Ufaransa Francois Hollande amekataa wito huo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ameliambia shirika la Habari la Reuters kuwa mzozo huo unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.