Michuano ya kuwania kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza Januari 2 hadi 12 mwakani, huku timu ya Simba ikijikuta katika kundi moja na waalikwa katika michuano hiyo timu ya Tusker kutoka Kenya.
Mashindano ya kuwania kombe la mapinduzi yalianzishwa na Shirikisha la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kwaajili ya kusherehekea kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar January 12 ya kila mwaka.
Mabingwa wa kombe la Kagame Yanga FC hawataweza kushiriki kwakusababu ya safari yao kuelekea Uturuki kwa maandaliza ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.
Azam ndio mabingwa watetezi wa Mapinduzi Cup, na mwka huu mshindi anapata Tshs million 10 na mshindi wa pili ni Tshs milioni 5.
Kundi A: Simba SC, Tusker FC, Bandari (Unguja) and Jamhuri (Pemba).
Kundi B: Azam FC, Mtibwa Sugar, Coastal Union, and Miembeni (Unguja).