Mafunzo Ya Online Journalism Kwa Waandishi Wa Habari Mkoani Rukwa Yameboresha Mahusiano Kati Ya Jeshi La Polisi Na Waandishi



Mafunzo ya online journalism kwa waandishi wa habari mkoa wa ruvuma yanaendelea kwa mafaniko, mafunzo hayo yanayosimamiwa na Union of Tanzania Press Club(UTPC) kwa kushirikiana na press club za mikoa, mafunzo hayo yamekuwa yakiwezeshwa na wawezeshaji ,Maggid mjengwa na Lukelo Mkami.

Ikiwa leo ni siku ya tatu kati nne za mafunzo ya waandishi wa habari wa mkoa wa rukwa yameonekana kuwa na tija kubwa kwa waandishi wa habari wa mkoa huu pamoja na jeshi la polisi wa mkoa wa rukwa, siku ya leo mkufunzi msaidizi ndg Lukelo Mkami nikiwa  na baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa huu tulitembelea makao makuu ya jeshi la polisi mkoani hapa na kuweza kukutana na Kamanda wa polisi Jackob Mwaruanda,

Katika mazungumzo yetu yaliyodumu kwa takribani dk 30, yalikuwa ni kuwa mazungumzo ya kumfahamisha kamanda wa polisi dhumuni la mafunzo haya na uwepo wa matumizi ya technologia ya kufikisha habari kwa wananchi kwa haraka na kwa eneo kubwa ikiwa ni pamoja na matumizi ya blogs na worldpress kwa waandishi wa habari ili kuweza kuwafikia wananchi hata walio nje ya mkoa huu mpaka nje ya mipaka ya Tanzania.

Katika mazungumzo yetu na kamanda wa polisi ambaye alionekana kufurahia uwepo wetu pale na kupendekeza baadhi ya mambo ambayo yatazidi kuimarisha  uhusiano wa jeshi la polisi na waandishi ambao kwa namna fulani umeonekana kama kulegalega, jambo kubwa sasa alilolizungumza amesema yupo tayari kushirikiana na waandishi ambao pia watakuwa na Blogs zao ili kuweza kuwafikishia wananchi habari kwa haraka na habari zenye ubora.

Hii ni hatua nzuri  ambayo ina nia ya kujenga taifa lenye uwazi na uwajibikaji.

Mkami Jr
Mjengwa Blog-Sumbawanga
Previous Post Next Post

Popular Items