Mheshimiwa Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na wageni toka Lichinga Msumbiji.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Balozi Hamisi Kagasheki(MB) akisalimiana na Wazee wa Jadi.
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) Akivalishwa Vazi la kijadi.
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akiweka Ngao .
Baadhi ya wazee wakiwa wameshika Silaha za Jadi walizotumia mababu zetu kupigania dhidi ya kupinga utawala wa Wakoloni wa Kijerumani
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiweka Sime.
Kamanda wa Jeshi la wananchi akiweka upinde
Mpiganaji wa vita kuu ya pili ya Dunia Mzee Komba akisindikizwa na kamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenda kuweka shahada ya uwa katika mnala wa mashujaa.
Hii ni kwa nje npyo hali ilivyokuwa
Mhe Balozi Hamisi Kagasheki(MB)Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na viongozi wengine wakitoa salamu ya heshima kwa mashujaa wa majimaji
Hapo wanajeshi wakiendelea kutoasalamuza maombelezi kwa njia ya kijeshi
Kuinamisha kichwa chini ni dalili ya kumwomba mwenyezi Mungu awaweke Mahali pema Mashujaa walioo tangulia Mbele zahaki
Katika kuwakumbuka Mashujaa waliotangulia mbele za Haki Jeshi la Wananchi limeweka Utaratibu Maalumu ikiwa ni pamoja na kulipua mizinga na Fataki katika kuwakenzi Mashujaa.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania likitoka nje ya Uwanja wa Mashujaa baada ya kumaliza taratibu zote za Maombolezo.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mzuri na wakuelimisha juu ya vita vya majimaji.
Moja ya wageni waliohudhuria toka mikoa mbalimbali pamoja na nchi jilani ya Mozambiq
Chief Emanuel Zulu akiweka shada katika kaburi la pamoja la mashujaa wa vita vya majimaji
Bw. Balthazali Nyamusya Mhifadhi Kiongozi Makumbuaho ya Taifa Maji Maji Songea
Hili ndilo Kaburi la halaiki walipozikwa mashujaa wa vita vya Maji Maji , watu waliozikwa hapa ni 66
Eneo hili walilozikwa mashujaa hawa limekuwa eneo muhimu.
Humu ni ndani ya Nyumba yenye vifaa vya kumbukukumbu na hapa inaonekana baadhi ya watu wakiona picha zenye vielelezo
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki akipewa maelezo juu ya Kaburi la Songea Mbano ambaye alizikwa peke yake na jina la Mji wa Songea limetokana na jina lake
Balthazar Nyamusya Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho Ya Taifa Maji Maji Sonhgea akitoa maelezo kwa
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) alipokuwa akizuru ukumbi wa historia ya vita vya maji maji.Miongoni mwa vionyeshwa katika ukumbi wa historia ni zawadi iliyokabidhiwa na MeyaAugusto Assique wa Jimbo la Lichinga kwa kutambua mashirikiano ya kihistia na kitamaduni
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) alipokuwa akizuru ukumbi wa historia ya vita vya maji maji.Miongoni mwa vionyeshwa katika ukumbi wa historia ni zawadi iliyokabidhiwa na MeyaAugusto Assique wa Jimbo la Lichinga kwa kutambua mashirikiano ya kihistia na kitamaduni
Wazee wa Kimila wakibadilishana mawazo juu ya uwelewa wa kila mmoja kuhusu vita vya Majimaji
Baad
Wanakikundi cha Better Life wakitumbuiza katika sherehe za kumbukizi la Mashujaa wa vita vya Maji MAJI
Pichani ni Balozi Khamis Kahgasheki9m(MB),Dkt Rehema Nchimbi mkuu wa mkoa wa Dodoma na Kepten mstaafu Aseri Msangi RC njombe.
Mkuu wa mkoa wa ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akiteta jambo na Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akiweka Ngao .
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma hukumbuka Mateso waliyoyapata Babu zao, Hapo wapo katika Viwanja vya Mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea kushuhudia Maombolezo yaliyoongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Saidi Thabit Mwambungu akisalimiana na Mjuukuu wa mpiganaji wa Vita kuu ya pili alishikana nae na pembeni yake ni Mzee Komba ambaye ndiye mpiganaji wa Vita kuu ya pili.
Baraza la Kimila la Makumbiusho ya Vita vya Majimaji wakitumbuiza,
Kikundi cha kucheza mziki wa kizazi kipya kikitoa burudani mbele ya wageni waliofika katika makumbusho
Nimoja ya wageno toka mikoa mbalimbali wakifatilia kwa makini kinachoendela uwanjani hapo
Mkuu wa Wilaya ya Binga Bi.Senyi Ngaga akifanya utambulisho wa baadhi ya viongozi
Kama inavoonekana katika picha hapo juu baadhi ya wazee wakiwa katika hali tofauti juu ya uchungu wa mateso waliopata ndugu zao
Huyo ni mchekeshaji maarufu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Chaku akitoa vitu vyake mbele ya jukwaa kuu
Hapo kila mmoja akisikiliza kwa hisia huku wengine wakiwa katika majonzi makubwa
Umati wa watu waliohudhuria katika katika tamasha la kumbukizi ya vita vya majimaji
wanafunzi wakisikiliza kwa makini juu ya historia ya vita vya majimaji iliyokuwa ikisomwa
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu akitoa maelezo juu ya Vita vya maji maji
Mama huyu kavaa vazi la magome ya miti ambalo vazi hili limetumia sana na wazee wa zamani ila kwa sasa vazi hili ni adimu
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB)akisoma hutuba
Dkt Rehema Nchimbi mkuu wa mkoa wa Dodoma akiwa na viongozi wengine wakipitia vitabu vya Wizara ya Maliasili na Utalii, Kitabu cha Maadhimisho ya kumbukizi ya vita vya Maji Maji Mkoa wa Ruvuma , Toleo la 1,mwaka 2006,2010-2012
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akitoa zawadi kwa mzee JJ gama tuzo kwa niaba ya bisiwajibu Gama ikielezea mchango wa vifaa alivyotoa kwa mchango wa makumbusho ya Taifa,
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akitoa cheti cha ushiriki kwa kampuni ya Mantra .
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akimkabidhi mwanafunzi zawadi ya ushiriki kwa kuchora picha zilizobeba ujumbe wa vita vya majimaji
Chiefu Emmanuel Zuru akiwa na Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB)
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akitoa cheti cha ushiriki kwa kundi la Better Life
Picha ya pamoja ya viongozi waliotoka mikoa mbalimbali
Balaza la wazee wa mila za kijadi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Makumbusho
.............................................................................
Maadhimisho ya Tamasha la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni Kitaifa yamekuwa yakiadhimishwa kila mwaka tarehe 27 Februari, Mkoani Ruvuma kuanzia mwaka 2010. Dhana ya maadhimisho haya ni kufanya Kumbukizi za Vita ya Majimaji ziwe kichocheo cha mabadiliko kwa jamii kifikra na Kiutamaduni. Kuwaleta pamoja wadau wa historia ya Vita vya Majimaji
Pia kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Maji Maji walionyongwa tarehe 27 Februari,1906 na Wajerumani ambao wamezikwa katika eneo la Makumbusho ya Kumbukizi ya Vita vya Majimaji – Songea
Vilevile Kutoa fursa kwa jamii kushiriki katika kuenzi na kuendeleza urithi wetu kupitia shughuli za kimila zinazofanywa na Wazee wa Baraza la Mila na desturi za jamii iliyohusika katika tukio la Vita vya Maji Maji.
Na kutoa elimu kwa Umma wa Watanzania kwa ujumla kuhusu Kumbukumbu za Kimakumbusho kupitia matukio ya kimila na kihistoria.
Kuweka dhahiri madhumuni ya kuanzishwa kwa Makumbusho ya Taifa nchini kwa vitendo.
Katika maadhimisho haya Waziri wa Mali asili na utalii Dkt.Hamis Kagasheki ameitaka jamii nchini kuenzi harakati hizo zilizofanywa na mababu wa taifa hili katika kupinga utawala wakikoloni.
Pia amesema amefurahishwa kuona kuwa maadhimisho ya kumbukizi ya vita vya majimaji yamekuwa na historia ya kuadhimishwa mwezi februari Mkoani Ruvuma katika ngazi ya mkoa tangu nchi yetu ipate uhuru, Hii imelenga kuwakumbuka Mashijaa wa Vita vya Maji Maji.
Hii imeonyesha kwa jinsi Uongozi wa mkoa , Wazee wa Baraza la Mila na Desturi na wananchi wanavyothamini mchango waliokuwa nao Mashujaa hawa hata kujitoa mhanga kutetea uhuru, haki na utawala wao pamoja na kulinda mila , tamaduni na rasilimali zilizopatikana kwenye maeneo yao kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Hili ni jambo la kuigwa na kila mtu kuthamini na kulinda urithi wetu wa utamaduni kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijazo.
Akiendelea kusema ameshuhudia kuwepo kwa taarifa za mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Mama Mkomanile ambaye alishiriki katika harakati hizo za mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni hivyo ni ishara kuwa akina mama nao walishiriki kikamilifu katika mapambano hayo dhidi ya ukoloni ambapo kwa upande wa Tanganyika ilikuwa ni Vita ya Maji maji ,na kwa upande wa Kenya ilikuwa ni Mau mau na vyote vilikuwa ni chanzo cha vuguvugu la ukombozi wa bara la Afrika.
Pia ametoa wito kwa wadau wa utafiti kufanya utafiti zaidi habari za mwanamke huyo ili nazo ziweze kuingizwa kwenye historia ya kumbukizi hiyo ya vita ya Maji Maji ambayo pia ilikuwa ni chachu ya ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla.