T.I na Young Jeezy wathibitisha kufanya album ya pamoja

Rapper Clifford Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I pamoja na Jay Wayne Jenkins a.k.a Young Jeezy wote kutoka Atlanta, Georgia wamethibitisha kurekodi album ya pamoja.

Tumekuwa tukiizunguzia kwa miaka mingi, lakini hatimaye tumeanza kuifanyia kazi” T.I aliiambia MTV News.
T.I ambaye mwezi uliopita alitumbuiza kwenye Fiesta ya Dar, amesema kuwa kwa sasa uwezekano wa kuikamilisha album hiyo ni mkubwa sababu kila mmoja amemaliza album yake binafsi.
“Usually, when we talking about it, either he’s working on finishing his album or I’m working on finishing mine. This is like one of the first times that we both putting our albums out around the same time. I’m done with my process, he’s done with his process, now we can collectively come together and do something together.”

Tip ameachia album yake iitwayo ‘Paperworks’hivi karibuni, album ambayo inakamata nafasi ya pili kwenye Billboard 200. Jeezy naye aliachia LP yake “Seen It All: The Autobiography” mwezi September.

Mpaka sasa T.I na Jeezy tayari wamesharekodi nyimbo zipatazo sita za album ya pamoja ambayo inasemekana inaweza ikaitwa “Dope Boy Academy”
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa