Lulu: Nitahukumiwa na Mungu

Mwigizaji anayekuja juu katika uigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu amekiri kuwa mfuasi mkubwa wa Biblia na mara zote haachi kusali.



Lulu alisema daima amekuwa katika hali hiyo ili kujiweka jirani zaidi na Mungu na ndiyo maana maneno mengi mabaya yanayosemwa na wabaya wake hayamwathiri kwa sababu yu karibu na Muumba wake.

“Daima nimejifunza kuwa karibu sana na Mungu na nasoma Biblia sana. Hilo limenifanya niwe na furaha kila siku kwa sababu najua Mungu ananipenda na ni yeye pekee anayeweza kunihukumu,” alisema.

Baadhi ya filamu zilizompaisha Lulu ni pamoja na Foolish Age, Family Curse, Family Tears, Ripe Tears na Confusion ambazo kwa hakika zinafanya vizuri sokoni kila kukicha.

Lulu anatuhumiwa kumwua mwigizaji maarufu Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake.
Previous Post Next Post