Fid Q kunyoa rasta zake!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Fid Q amesema yupo mbioni kupunguza rasta zake kwa lengo la kujiweka tofauti na jinsi ilivyo. 



Mwanamuziki huyo alisema kimsingi akishamaliza kupunguza rasta, atanyoa kabisa nywele zake kwa mtindo wa unga na alipoulizwa zaidi alisema anataka kujibadilisha ili aongeze pia mashabiki wake.

Alisema si jambo la kwanza kwa wasanii kuamua kubadili staili zao za mavazi au mitindo ya nywele na mara nyingi ushahidi unaonyesha kuwa kwa kufanya hivyo hata muziki nao soko lake linapanda.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa