David Moyes apewa nafasi Hispania

David Moyes amepewa nafasi ya kurudi kwenye soka na Real Sociedad ya Hispania.

Klabu hiyo ya Hispania ilimfukuza kocha Jagoba Arrasate siku ya Jumapili baada ya kufungwa na Malaga siku ya Jumamosi, na wamemgeukia kocha wa zamani wa Manchester United na Everton.

Kwa sasa Moyes yupo nchini Qatar, ambapo anafanya kazi BeIN Sports, na inaeleweka kuwa anafikiria nafasi hiyo.



Ila Mskoti huyo 51, inafahamika kuwa ana tahadhari kubwa kwani anajua kazi ijayo inahitaji mtu sahihi baada ya kipindi kigumu cha miezi 10 Old Trafford.

United walikuwa wakitetea ubingwa wa Ligi Kuu wakati Moyes alipofika lakini aliipeleka hadi nafasi ya saba, akikosa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 1995-96.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa