Beef la Tyga na Drake lazidi kukua

Wasanii wawili waliopo katika kundi moja la YMCMB Tyga na Drake sasa lile beef limezidi kuchukua sura mpya na kumhusisha mwanadada aliekua na mahusiano na Tyga aitwae Black Chyna.

Mwishoni mwa juma lilipoita Tyga alianza kupost katika Instagram picha iliomuonesha akiwa sambamba na msichana toka katika familia ya kina Kardashian aitwae Kylie Jenner wakiwa katika mavazi maalum ya sherehe ya kila mwaka ya huko Marekani ya Halloween.



Baada ya picha hiyo Black Chyna alijitokeza na kuanza kuanza ku-like picha za Drake hatua iliomkasirisha Tyga na kuanza mashambulizi ambayo yalilenga kuelekea akisema huyo si kahaba wangu.

Drake alijibu mashambulizi ya kudhihaki baada ya kuweka picha ya pili iliomuonesha yeye akiwa na Kylie Jenner kwa nyuma yake ambapo ilifuatiwa na picha nyingine aliyopost Black Chyna akiuliza kua umenimiss? kamwe hautanisahahu na mfululizo wa tweets nyigine za malumbano.

Katika Tweets zingine mwanadada Black Chyna alisema kwamwe hakuwahi kumpenda Tyga bali alikua anafuata hela zake tu lakini alikri kua alimchukua katika klabu za wachojoaji nguo na kumpatia familia nzuri na pia alimsaidia kupunguza tabia yake ya ulevi.

Ndo hivyo lakini tunaomba wasije wakafikia ya akina 2Pac na Big Poppy.
Previous Post Next Post

Popular Items