Wakazi aanza kuuza mziki wake Itune

Rapper Webiro Wakazi aka Swag Bovu amepiga hatua nyingine katika biashara ya muziki kwa kuongeza njia ya kujiingizia kipato kimuziki ambapo hivi sasa nyimbo zake zinapatikana iTunes.




Wakazi aliseema kuwa hii ni hatua kubwa kwake ikiwa ni kati ya mipango yake ya muda mrefu tangu akiwa nje ya nchi kuhakikisha nyimbo zake zinaingia kwenye soko la kimataifa hata kwa njia ya mtandao.

Akizungumzia njia alizotumia kufanikisha zoezi hilo, Wakazi amesema sio njia ngumu ila ni njia ndefu.

“Process sio ngumu ila ni ndefu. Sasa unajua watu wengi hawana subira ile…wakiambiwa fanya hivi, leta kile wanaweza kuvunjika moyo,” Wakazi aliiambia tovuti ya Times Fm.




“Ila ni process ambayo ni rahisi tu ambayo mtu yeyote anaweza akaenda akafuatilia kwenye mtandao wao au akafanya kwa kutumia distributers ambao wanafahamika kwamba wao ndio huwa wanazipeleka zile nyimbo wanafanikiwa,” Ameongeza.

Katika hatua nyingine, rapper huyo amesema kuwa wiki hii ataachia nyimbo tatu kwa mpigo kwa ajili ya mashabiki wake. Wakazi amepanga kuwashibisha burudani mashabiki wake ambapo wiki ijayo amepanga kuachia video ya wimbo wake mwingine mpya.
Previous Post Next Post