Manchester City imeifunga Hull City jumla ya magoli 2-0 katika uwanjani wake wa Etihad ,lakini licha ya ushindi huo kiwango chake kilikuwa si cha kuridhisha sana.
Alikuwa ni Alvaro Negredo aliyetoka benchi kuanza kuipatia Man City goli la kwanza huku Yaya Toure kufunga bao la pili kwa mkwaju wa free-kick aliopiga kwa ustadi mkubwa.(P.T)
Hull iliweza kupata nafasi kubwa za kufunga bao katika kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji Sone Aluko alishindwa kumalizia katika lango lililokuwa limeachwa wazi na kipa Joe Hart.
Manchester City ilionekana bado kutetereka katika safu yao ya ulinzi baada ya kukosa tena huduma za mlinzi Vicent Kompany ambaye bado anauguza jeraha.
Tags:
Sports