Walichotamka JWZ kuhusiana na Wananchi wanaovalia sare Jeshi, Je Tamo hilo linawalenga Diamond, Ney wa mitego na Chegge!

Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, Jumatatu ya wiki hii lilitoa tamko kuhusu wananchi kumiliki au kuvaa sare za jeshi hilo.


Ingawa tamko hilo la JWTZ limetoka kwa ufupi bila kuweka wazi kwanini wameamua kulitoa tena wiki hii!


Ni Jambo lisilofichika  kuwa limetokana na wasanii kadhaa wakiwemo Diamond Platnumz  na dancers wake, Chege na Nay wa Mitego kuvaa sare hizo kwenye show ya Serengeti Fiesta iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.




Kuna tetesi kuwa wasanii hao walipewa kibali maalum kutoka jeshi hilo kufanya hivyo. Kama walimpa kibali Diamond na wasanii wengine, tunadhani lilikuwa ni jambo jema kama jeshi hilo lingeweka wazi kuwa walitoa kibali kwa wasanii hao kutumia sare zao.

Ama kwenye taarifa hiyo fupi kwa vyombo vya habari walipaswa kusema kuwa ‘mwananchi anaweza kutumia sare hizo katika matumizi yake iwapo atakuwa na kibali maalum kutoka JWTZ’. Iweje leo umwambie mwananchi kuwa asimiliki wala kuvaa sare hizo wakati jana tu aliwashahudia wasanii wakiwa wamezivaa jukwaani?



Na mbona kama jeshi linakatakaza, kwanini hatujasikia hatua yoyote imechukuliwa kwa wasanii hao? Mbona kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, jeshi halijasema kuwa Diamond na wasanii wengine wamefanya kosa? Au akifanya msanii anayejulikana hilo sio kosa?

Kama walipata kibali kwanini JWTZ halijasema hivyo ili tufahamu kuwa nguo hizo zinaweza kuvaliwa pale tu kibali maalum kitakapotolewa! Taarifa hiyo iliyotoka haijaweza kujibu maswali muhimu waliyonayo wananchi wengi kuhusiana na uhalali wa kuvaa sare za kijeshi. Ilitakiwa kuja na ufafanuzi kwa kina na sio wa aya mbili zisizojitosheleza.

Previous Post Next Post

Popular Items