Umoja wa Mataifa umekataa rasmi madai ya fidia ya watu walioambukizwa ugonjwa wa Kipindupindu nchini Haiti, kufuatia kulipuka kwa ugonjwa huo na kuua zaidi ya watu elfu nane(8,000) na wengine kwa maelfu kuugua.
Umoja huo umesema una kinga dhidi ya mashitaka ya aina hiyo.
Hata hivyo ushahidi umeanza kufichuka kuwa ugonjwa huo uliingia nchini humo kutoka katika kambi ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa, kufuatia kupasuka kwa mabomba ya kusafirisha maji machafu.