Victoria Kimani athibitisha kutoa burudani katika Serengeti Fiesta Dar

Mwanadada anayefanya vizuri katika indusrty ya muziki kenya na Bongo Victoria Kimani anatarajia kuungana na mastaa kibao wakiwemo rapper wa Marekani, T.I., msanii wa Nigeria, Waje na wasanii wengine wa Tanzania kwenye kilele cha Serengeti Fiesta 2014 jijini Dar es Salaam.



Kupitia Instagram, Victoria Kimani amesema ana furaha kubwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza.

“BONGO ! I’M SO EXITED TO BE PERFORMING AT THE 2014 SERENGETI. See you soon! Oct. 18th – Leaders Club #TANZANIA Nakupenda Sana.”
<

Hata hivyo wasanii mbalimbali kutoka nje ya Tanzani akiwemo T.I. wanatarajiwa kuanza kuingia Dar Ijumaa hii.
Previous Post Next Post