T.I. kufanya kitu kikubwa, kuzindua mavazi yake jijini Dar es Salaam

T.I  ndiye msanii anayekuja Tanzania katika kukamilisha kilele cha Tamasha kubwa la Serengeti Fiesta,  T.I ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy kwa mwaka 2014 .

Katika siku ya leo  imetangazwa rasmi kuwa mavazi ya T.I ya Hustle Gang, Akoo pamoja na Strivers Row nayo yatazinduliwa rasmi katika duka la Pop Up Shop lililopo katika super market ya Dar Free Market siku ya tarehe 18-October, 2014.





Akizungumzia uzinduzi huo wa mavazi ya T.I, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Grand Hustle Records, Jason Geter ambayo ndio kampuni inayomsimamia msanii B.O.B na mwanadada anayekuja kwa kasi Iggy Azalea, alisema anaamini soko la Tanzania na Afrika kwa ujumla ni masoko makubwa kwa bidhaa zao.

‘Tuna matarajio makubwa kuhusiana na kuleta bidhaa zetu nchini Tanzania, na tunatarajia sio tu kuleta bidhaa zetu hapa nchini, bali kwenda mbali zaidi kwa kujifunza soko la mitindo hapa nchini’ alisema Geter.

Duka la Pop Up litafunguliwa kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saa tisa mchana ambapo wateja watapata fursa ya kununua nguo halisia za Hustle Gang, Akoo na Strivers Row Clothing, huku wamiliki wa maduka wakiweza kutazama bidhaa tofauti na kuagiza oda zao.

Tamasha la Fiesta ambalo linajulikana kama tamasha kubwa na lenye mafanikio zaidi kwa Afrika Mashariki na Kati likiwa na wahudhuriaji wasiopungua 500,000 kwa mwaka huku likijivunia wasanii wakubwa waliowahi kutoa burudani miaka ya nyuma kama Ludacris, 50 Cent, Rick Ross na wengineo.

Mwaka huu kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta kitafanyika tarehe 18 mwezi wa kumi katika viwanja ya Leaders jijini Dar es Salaam.
Previous Post Next Post