Umeiskia hii ya Elton John kumsifu Papa Francis kwa kukubali mashoga Kanisa Katoliki

Elton John alimuita Pope Francis ‘shujaa wangu’ katika shughuli ya kuchangisha fedha za UKIMWI kwa huruma zake na kuhimiza mashoga kukubalika katika kanisa Katoliki.

Mwimbaji huyo wa Rocket Man alihodhi tukio hilo kupitia wakfu wake wa Elton John AIDS Foundation, siku ya Jumanne jijini New York.

Elton John alisema; “Miaka kumi iliyopita moja ya tatizo kubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI ilikuwa Kanisa Katoliki. Leo tuna Papa anayezungumzia suala hili.”



Maaskofu wa Katoliki waliweka historia kwa kuwakaribisha mashoga mapema mwezi huu, na kuonyesha mabadiliko ya kina mwishoni mwa mkutano wa wiki mbili ambao ulionekana kuneemeshwa zaidi na Papa Francis baada ya Katoliki kuwa na mawazo mgando.

Ila Francis mwenyewe, wakati akisisitiza kuwa vitendo vya ushoga ni dhambi, mwaka uliopita kilikuwa kipindi cha uvumilivu kwa fikra za Vatican baada ya kuzungumza kuutetea ushoga.

Ila juhudi za Francis hazijasahaulika. “Ni mtu mwenye huruma, upendo ambaye anataka kila mtu kuwepo katika upendo wa Mungu,” alisema John.


Elton John amemtaja Papa Francis kama “shujaa wake” kwa kitendo cha kukubali mashoga katika kanisa Katoliki.

Ni jambo la kuogopesha kwa kile anachojaribu kukifanya dhidi ya wengi, watu wengi kanisani wanakipinga. Ni mjasiri na shujaa, na hicho ndicho tunachokihitaji katika dunia ya leo”.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa