Mzee majuto ajipanga kufanya filamu na Diamond platnumz akiwa na wema

Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto amesema hivi kariburi alimshawishi Wema Sepetu azungumze na mpenzi wake Diamond Platnumz ili wafanye kazi ya pamoja.



Diamond na Mzee Mjuto

Mzee majutoa alisema kuwa amemwahia kazi wema Sepetu ili aweze kuzungumza na mzee (Diamond)

“Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja,” amesema Majuto. “Mimi, Wema na Diamond, hata Diamond ninaweza kuzungumza naye sema nimeanza na Wema kwanza, akikubali mtasikia tu.”

Kwa upande mwingine Majuto amesema ili acheze filamu anahitaji kulipwa shilingi milioni 3.

“Umri unaenda sasa biashara za nisaidie nisaide hakuna, kama unanitaka ili tufanye kazi unatakiwa uandae milioni 3.”
Previous Post Next Post

Popular Items