Mwasiti kushoot video mbili mpya kimataifa zaidi, kutumia mbinu hizi...

Mwanadada aliyeimba wimbo wa ‘Mapito’ Mwasiti Almas amesema yupo mbioni kuanza kushoot video zake mbili ambapo moja atashoot na Adam Juma na nyingie na Nick Dizzo.




Mwasiti amesema ilikuwa aachie kwanza single ya wimbo ‘kisigino’ lakini ameshindwa kutokana na majukumu ya kikazi.

“Nafanya video so soon kwasababu bado nipo kwenye safari kwahiyo nashindwa kutoa hizo kazi, ila kibubwa zaidi nasubiria nikipata nafasi ndogo tu nitaanza kushoot video, tena nitashoot video mbili ili kukata kiu ya muziki ya mashabiki wangu. Kwahiyo wadau wangu wakae mkao wa muziki mzuri,” alisema Mwasiti.

Katika hatua nyingine Mwasiti alizungumzia njia yake atakayoutimia ili kuupeleka muziki wake kimataifa bila kupitia njia ambazo wanatumia wasanii wengi.

“Plan yangu kubwa sana, unajua mimi plan yangu sio kibongoflava zaidi, kwahiyo mimi plan yangu katika muziki ili kwenda kimataifa ni kufanya matamasha makubwa sana, sio kukutana kwenye show sijui wapi na wapi hapana! Mara nyingi naangalia show zangu nyingi ziwe za matamasha. Kuna wanamuziki wakubwa wa Tanzania hamuwaoni wakifanya hizo show za kawaida, kumbe nimegundua nje ya mipaka yetu wanafanya mambo makubwa sana. Huu ni mtazamo katika muziki ili uende kimataifa kwa kutumia njia tofauti na ambao wanazitumia wasanii mbalimbali, mimi nitakuwa nikiomba kushiriki katika matamasha makubwa ambayo na hakika yatanifikisha mbali sana,” alisema Mwasiti.



Previous Post Next Post

Popular Items