BBA: Laveda awa ‘Head of House’ wa kwanza ni mshiriki kutoka Tanzania

Shindano la Big Brother Africa Hotshots limezinduliwa Jumapili hii, jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.


Msimu wa mwaka huu umezinduliwa kwa washiriki wote 26 kuonesha vipaji vyao na watazamaji kuwapa marks. Mwakilishi wa Tanzania, Laveda ndiye aliyeongoza kwa kupata asilimilia 85 kwa uhodari wake wa kupiga saxophone. Ushindi huo umemfanya Big Brother amtangaze kuwa ‘mkuu wa nyumba’ au ‘head of house’ wa wiki ijayo na hivyo kuwa mshiriki pekee ambaye hatakuwa kwenye hatari ya kupigiwa kura kutoka. Washiriki wengine wote 25 wiki ijayo watakuwa kikaangani kutoka Jumapili.

Mkenya Sabina amekamata nafasi ya pili kwa kupewa asilimia 72 kutokana na vichekesho alivyovitoa. Mwakilishi mwingine wa Tanzania, Idris amepata asilimia 62 kwa kucheza jukwaani.

Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye uzinduzi huo. Shindano la mwaka huu litadumu kwa siku 63 pekee. Mshindi wa BBA atazawadiwa $300,000.
Previous Post Next Post