Lundenga na Sitti Mtemvu 'Miss Tz' wazungumza na waandishi wa ahabari , Ukweli wa umri wa miss Tanzania uko hapa

Waandaji wa shindano la Miss Tanzania 2014 Lino International ambao wakishirikiana na Redds wamekutana leo jijini Dar es salaam na waandishi wa habari ili kuzungumza nao kuhusu skendo ya umri halisi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.Mkurugenzi wa Lino nternational Agency Hashim lundenga amesema tuhuma za kuwa miss Tanzania anamtoto sio kweli na kwamba hairuhusiwi kwa mshindani wa Miss Tanzania kuwa na Mtoto. Pia Hashim ameonyesha vyeti halisi vya kuzaliwa vya Sitti abavyo vimeonyesha amezaliwa 31,May,1991.
Yafuatayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti Mtemvu mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu kudanganya umri, elimu na mambo mengine.


Haya ndiyo waliyoyasema  Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti’  alsema Lundenga
Cheti cha Kuzaliwa
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa’  alsema Lundenga

‘Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo huo’  alsema Lundenga


Passport
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda’ –  alsema Lundenga
‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana, katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′  alsema Lundenga
‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original’ alsema Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu’  alsema Lundenga

Baada ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara’ -alisema Miss Tanzania
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ – alisema Miss Tanzania
Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema  ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli’
Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. 
kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA