Irene Uwoya, Baba Haji habari ya mjini

NYOTA wa sinema za kibongo, Irene Uwoya na Adam Haji ‘Baba Haji’ wamekuwa gumzo jijini Dar es Salaam baada ya filamu ya Kitoga waliyoigiza kama wapenzi waliotoka familia ya kimasikini na tajiri kuonekana kupokelewa kwa mikono miwili na wadau sinema za Tanzania huku wakisema walionyesha uhalisia zaidi.



Wasanii hao walisema kwa nyakati tofauti kuwa juzi ilikuwa ya usumbufu kwao kwani walipigiwa simu za kupongezwa na mashabiki wao ikiwa ni muda mfupi tangu filamu hiyo kuingizwa sokoni na ilikuwa inasubiriwa kwa muda mrefu na wadau wa sinema za Bongo.

Uwoya alisema hiyo ni ishara kuwa ujumbe umewafikia Watanzania wengi na wapenda filamu kwa ujumla.
Previous Post Next Post