Diamond achafuka Nigeria

Amini usiamin dunia sasa ni kama kijiji, Kesi inayomkabili msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Naseeb ‘Dimond’ akituhumiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuvaa sare za jeshi hilo sasa imetua pia kwa mashabiki wake nchini Nigeria.

Diamond Platnumz alipanda jukwaa la Serengeti Fiesta akiwa amevaa sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambapo ni kinyume cha sheria.

Mitandao mbalimbali nchini humo imekuwa na habari za Diamond na mingi ikihoji hatima ya mwimbaji huyo aliyejizolea umaarufu katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa upande wake, mtayarishaji maarufu wa muziki jijini Lagos, JJ Romantic alikaririwa akieleza kusikitisha na tukio hilo, huku akisema kuwa kwa namna anavyomkubali 

Diamond angependa kuona suala hilo linaisha mapema pasipo madhara makubwa.


Via:Taarifa
Previous Post Next Post