Ommy Dimpoz ' Sijawahi kwenda kwa Mganga kutafuta Mafanikio'

Msanii wa bongo flava nchini na hit maker wa Ndagushima, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz, ameruka kimanga kuwatumia waganga wa kienyeji ili kufanikisha kuvuma kwa kazi zake kisanii.


Dimpoz ambaye ni mmoja wa wanamuziki wanaotamba katika muziki huo katika Afrika Mashariki na Kati amesema hana wazo la kutumia nguvu za giza ili apate mafanikio katika uimbaji.

Alisema kabla na baada ya kuanza muziki hajawahi kwenda kwa waganga kusaka ndumba ili kupata mafanikio kwani anaamini kila kitu ni mipango ya Mwenyezi Mungu.

Msanii huyo aliongeza kuwa mafanikio aliyonayo yanatokana na utashi wake pamoja na kufuata malezi na imani aliyonayo mbele ya Muumba wake na si kutegemea nguvu za giza kwa vile hata familia yake haijawahi kuwa katika mfumo huo.


Previous Post Next Post