Davido ndiye msanii pekee wa Afrika aliyechaguliwa kuwania tuzo za ‘Soul Train Awards 2014’ Marekani

Hit Maker wa SKELEWU na Aye, Davido ametajwa kuwania kipengele cha ‘Best International Performance’ kupitia hit yake ‘Aye’ kwenye tuzo za ‘Soul Train Awards 2014′ zilizopangwa kutolewa November 7 huko Las Vegas, Marekani na baadae kuoneshwa kupitia Centric na BET November 30. Davido ndiye msanii pekee wa Afrika aliyetajwa kuwania tuzo hizo.


Katika kipengele hicho Davido anachuana na Shaggy feat. Ne-Yo kupitia ‘You Girl’, pamoja na Ziggy Marley – I Don’t’ Want To Live On Mars.
Best International Performance Nominations


Davido – Aye
Machel Montano – Ministry Of Road (M.O.R.)
Nico & Vinz – Am I Wrong
Sam Smith – Stay With Me
Shaggy feat. Ne-Yo – You Girl
Ziggy Marley – I Don’t’ Want To Live On Mars

Wasanii wakubwa wakimataifa waliotajwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Chris Brown ambaye anaongoza kwa kupata nominations 7, akifuatiwa na Beyonce mwenye nominations 6 na Pharrell Williams akiwa na nominations 5.

Previous Post Next Post