Beat ya ‘Ole Themba’ ya Linah ilikuwa itumike kwenye wimbo wa Davido na Mafikizolo ‘Tchelete’


Hit maker wa ‘Ole Themba’, Linah Sanga amesema beat ya wimbo huo, Ole Temba ilikuwa itumike kwenye wimbo wa Davido na Mafikizoro, Tchelete.




Linah amesema baada ya kupewa achangue beat alichangua beat hiyo ya ‘Ole Themba’ ambayo Davido na Mafikizolo walishaanza kuifanyia mazoezi.

“Nimefika studio unakuta beat nyingi producer anakusikilizisha beat nyingi,” amesema Linah. “Kwahiyo tumefika studio kama kawaida akatusikilizisha beat zote ikafikia beat ya Ole Themba tukaipenda, tulivyoipenda producer akacheka sana! Tukamwambia ‘kwanini unacheka’, ‘Mnajua hii beat mliyochagua inataka itumike na mastaa wakubwa sana hapa Afrika’. Alivyoongea vile sikujua kwanini anaongea hivyo,” aliongeza.




“Mimi kwa uelewa wangu nilihisi mimi ni msanii mdogo, lakini akaja akasema ‘una bahati sana kwa sababu umependa hii beat na hii beat ilikuwa ya mastaa wakubwa hapa Africa, nikitutengezea wimbo lazima ufanye vizuri.’ Ndo tukamuuliza ‘beat ilikuwa ya nani?’ Akasema ‘hii beat ilikuwa ya Davido na Mafikizolo, ule wimbo wao Tchelete walikuwa waimbie mle kwenye beat ya Ole Themba’. Kwahiyo Davido alivyoondoka akarudi akaja na idea yake nyingine akajaribia kuimbia kwenye Ole Themba ikagoma kwahiyo wakaamua waniachie tu mimi nifanye.”

Previous Post Next Post