Steve Nyerere ajiuzulu uenyekiti Bongo Movies

Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Steve Nyerere aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movies ameamua kujiuzulu nafasi hiyo.

Steve ameeleza uamuzi wake kupitia Instagram bila kutoa sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake.


“Napenda kuwashkulu ndugu zangu wote wasaniii wenzangu kaka zangu mama zangu rafiki zangu mimi pamoja na family yangu nimeamua kujiuzuru uongozi wa bongo move nabaki kuwa mwanachama wa kawaida naimani tulifurahi pamoja tukauzunika pamoja na daima tutakuwa pamoja.”

Uamuzi wa Steve Nyerere umepokelewa kwa hisia tofauti na wapenzi wa filamu za kitanzania ambao wengine wamemtaka kutofanya hivyo huku wakitaja ‘majungu’ na kusemwa kama chanzo cha yote.

“Khaaaaaaa asa @stevenyerere2 kujihuzur sio suluhisho la tatizo kaanza willy umefata ww sasa c kamat nzima itajiuzur!?? Why mnashindwa kukaa km wasanii mkasuluhisha penye makosa mambo yakaendelea? Majungu yapo kila sehem kusemwa kupo kila sehem @stevenyerere2 mnapoelekea bongomovie kila mtu atakaa mwenyewe wallah.” Ameandika shabiki anaetumia jina la Neyjd.
Previous Post Next Post