Kwa wadau wetu wanaosoma makala hii sijasema wala kumaanisha uache chuo! ila fikiria kwa kina utaleta tofauti gani kwa kile unachofanya, na je mafanikio yako umelenga kwenye nini? Je unaweza Kujifunza kitu gani kutoka kwa hawa watu? na kuleta changamoto zipi katika jamii yako?
Inawezekana komputa za Mac na bidhaa nyinginezo kama iPhone zisingekuwepo kama Steve Jobs angebakia chuo.
Jamaa huyu aliacha chuo pale Ripon College siku chache kabla ya kumaliza. Ni moja ya watu waliofanya vitu vikubwa kwenye filamu za Star wars miaka 1977.
1. STEVE JOBS
2. Bill Gates
Moja wa watu walioacha chuo Harvard na wamefanikiwa na ni tajiri mkubwa duniani. Mwanzilishi wa Microsoft. Kauli aliyoitoa kwenye mahafali pale Harvard mwaka 2007 alisema ” Mimi ni mshawishi mbaya ndio maana mmeniita niongee wakati wa mahafali. Ningeongea wakati wa kuanza masomo yenu ni wachache sana mngekuwepo hapa.”
3.Frank Lloyd Wright
Mbunifu mkubwa wa vyuo vingi marekani lakini hajawahi kuhudhuRia hata kimoja. Ingawa Frank Lloyd Wright alichaguliwa kwenda chuo cha Wisconsin-Madison mwaka 1886, lakini aliacha baada ya mwaka mmoja.
4. Buckminster Fuller
Bwana Huyu alifukuzwa Harvard mara mbili lakini ni mtu ambaye amefanikiwa sana na kuleta mawazo mapya katika ulimwengu huu. “He was expelled from Harvard twice: first for spending all his money partying with a vaudeville troupe, and then, after having been readmitted, for his “irresponsibility and lack of interest.”
5. James Cameron
Muongozaji maarufu wa filamu za Hollywood aliyetengeneza filamu nyingi za kubuni na za kisayansi na zenye gharama kubwa zikiwemo Titanic na Avatar.
6. Mark Zuckerberg
Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook na aliyekuwa mwanafunzi wa Harvard. Baada ya Facebook kuanza kupata umaarufu aliamua kuacha chuo.
7. Tom Hanks
Mwigizaji maarufu aliyeamua kuacha chuo Sacramento State na kujiunga na Great Lakes Theater Festival kule Cleveland, Ohio. Huko akajifunza vitu vingi kumfikisha kuwa moja ya waigizaji na watengeneza filamu maarufu huko Hollywood.
8. Harrison Ford
Jamaa huyu aliacha chuo pale Ripon College siku chache kabla ya kumaliza. Ni moja ya watu waliofanya vitu vikubwa kwenye filamu za Star wars miaka 1977.
9. Lady Gaga
Kabla ya kuwa Gaga, alikuwa anaitwa Germanotta. alizaliwa na Stefani Joanne Angelina Germanotta, msanii ambaye kwa sasa anaitwa Lady Gaga alianza kusoma New York University’s Tisch, Shule ya Usanii na baada ya hapo aliacha chuo baada ya mwaka mmoja na kuanza uimbaji wake pale New York club na kuweza kusaini mkataba wake na Interscope Records akiwa na miaka hiyo hiyo 20.
10. Tiger Woods
tu maarufu katika mchezo wa golf, baada ya miaka miwili aliacha kusomea uchumi pale Chuo cha Stanfold, kwa sasa analipwa zaidi ya dola milioni 100 kwa mwaka.
Chanzo cha habari (Time)