Scotland yakataa kujitenga na Uingereza

Wananchi wengi wa Scotland waliopiga kura katika zoezi la kuamua endapo nchi hiyo iwe huru na ijitenge na Uingereza au la, wameamua kuwa nchi hiyo iendelee kuwa sehemu ya Uingereza.

Asilimia 55 ya watu wote waliopiga kura wameamua kubaki katika muungano na Uingereza.



Waziri wa kwanza wa Scotland, Alex Salmond ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuwashawishi raia wa Uskochi kupiga kura ya ‘Ndiyo Uskochi iwe huru’, amekubali matokeo hayo na kueleza kuwa idadi kubwa ya watu waliopiga kura kusapoti harakati hizo haitakiwi kubezwa hata kama imeshindwa na kwamba hii ni ishara kubwa kwa miaka ijayo kuwa itawezekana.


Wananchi waliosapoti upande wa 'Hapana' wakisherehekea ushindi

Salmond amewataka upande ulioshinda kuhakikisha wanatimiza ahadi walizozitoa kwa wananchi wakati wa kampeni.

Previous Post Next Post