Mwisho mwampamba na mkewe Mnamibia Meryl wa ‘BBA’ wapata mtoto pili

Mwisho Mwampamba ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha ‘Boys Boys’ cha TV 1na mkewe Meryl ambaye walikutana na kuanzisha mahusiano kwenye Big Brother Africa ‘All stars’, wamefanikiwa kupata mtoto wao wa pili kama couple.


Meryl ambaye ni Mnamibia amejifungua mtoto wa kiume mwishoni mwa May 2014 ambaye wamemuita ‘King David’.



Meryl akiwa na mtoto wa Mwisho (King David)

Mwisho na Meryl ambao walifunga ndoa mwaka 2011 walifanikiwa kupata mtoto wa kwanza wa kike 2012.

Couple hiyo sasa ina jumla ya watoto wanne, wawili waliowapata kwenye ndoa na wawili waliowapata kabla ya kukutana, mmoja wa Meryl na mmoja wa mwisho.

Cha kufurahisha zaidi katika familia hiyo ni majina ambayo ambayo wamewapa watoto wao waili, mmoja anaitwa ‘Monkey’ na mwingine anaitwa ‘Happy feet’ ambaye ndio mtoto wa kwanza kuzaa na Mwampamba.
Previous Post Next Post