Picha: Kili Music Tour Tanga ilivyofana

Tamasha la Kili Music Tour limekamilisha awamu ya kuzunguka mikoani kwa show iliyofana katika uwanja wa Mkwakwani Tanga. Tamasha hilo linalidhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager lilipambwa na burudani toka kwa wasanii wanaofanya vizuri nchini wakiongozwa na malkia wa mipasho Khadija Kopa na mfalme wa taarab Mzee Yusuph ambao waliongoza kundi la wasanii kumi kutoa burudani kwa wakazi wa Tanga.

Dulla wa EATV akiendesha shindano kwa mashabiki wa kike waliojitokeza kwa wingi uwanjani

Tamasha hili sasa linarejea jijini Dar es Salaam ambapo Jumamosi Septemba 6 litahitimishwa katika viwanja vya Leaders Club.


Backstage: Nikki wa Pili na Ommy Dimpoz


 Ommy Dimpoz na madansa wake wakifungua rasmi burudani ya Kili Music Tour mkoani Tanga



 Ben Pol mmoja ya wasanii walioshangiliwa sana katika usiku wa Kilimanjaro Music Tour akiwa jukwaani



 Mkongwe wa Hip Hop Profesa Jay akisikiliza kelele za mashabiki waliokuwa wakiimba wimbo wake wa zari la mentali

 Mashabiki waliofurika uwanja wa Mkwakwani Tanga wakishangilia mara baada ya Kili Music Tour kukamilikam



 Mfalme wa Taarab nchini Mzee Yusuph akiifunga burudani uwanja wa Mkwakwani
 Malkia akifurahia burudani toka kwa mfalme

Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA